Karibuni sana kwenye ukurasa wetu wa intaneti 
Jina la „enkaina-e-retoto“ yaani „mikono saidizi“ ni jina la kikundi
cha marafiki, ambao wapenda sana kuwasaidia wamasai na utamaduni wao kwa
kushirikiana nao wenyewe na kuwaunga mkono…
… kwa habari zaidi tazama "sisi ni nani"
Mabadiliko ya hali ya hewa po pote duniani/pamoja na hali za ukame ambazo
hutokea zaidi na zaidi duniani zinadhuru hata kabila fahari la wamasai. Maradhi
ya mifugo, pengine matatizo ya kiekolojia zinawashawishi wamasai waache zaidi na
zaidi namna ya utamaduni wao ya zamani. Wamasai wanatafuta njia za kujipatia
nafuu kwa kushirikiana na maafisa wenyeji na mashirika ya misaada mbalimbali.
Lakini jitihada yoyote ile kama vile ardhi ya pori ya wamasai itumike zaidi kwa
ukulimo fulani huletea hata matatizo mengine kadha na husababisha madhara kwa
namna wamasai walivyozoea kuishi tena madhara mabaya kwa mazingira yao...
… kwa habari
zaidi tazama "maarifa zaidi"
Hali ya njaa ama hali ya kutopata malisho yaliyo kamili ambayo inatokana na ukame na
shida zingine, inasababisha magonjwa mbalimbali yanayodhoofisha hasa wale
wasio na uwezo miongoni mwa jamii ya kimasai, kama vile akina mama na watoto wao.
Mashirika na serikali ya Tanzania kwa kujenga hospitali na vituo vya matibabu,
zinajitahidi sana kuboresha uhudumu wa afya kote nchini. Lakini wamasai kwa kulingana
na mila yao wamezoea kutumia dawa za mitishamba hasa. Kutokana na jitihada za
wamasai wenyewe, tena kwa kushirikiana nao wenyewe katika miradi yenye
malengo maalumu - kikundi chetu kiitwacho "enkaina-e-retoto" kinataka kuwaunga
mkono wamasai hata katika kazi ya kujenga vituo vya matibabu ambapo dawa
za asili mbalimbali zitokanazo ulimwenguni popote zitapatikana, na vilevile
yapatikanapo madawa yanayokunsanyika na kutengenezwa umasaini yenyewe…
… kwa habari zaidi tazama "miradi yetu"
Wamasai ndio wataalamu wenyewe hasa kuhusu dawa za mitishamba na utengenezaji
wa chai asili kutokana na majani na mimea maalumu inayostawi katika baadhi ya
sehemu umasaini. Wamasai huvuna mizizi ama majani hayo ya chai aslili kwa
uanghalifu na bila uharibifu wa mazingira na wanakubali kuuzia mavuno hayo
kupitia kikundi chetu cha "enkaina-e-retoto", ili yapatikane hata katika nchi za
ng'ambo kama vile huko Ulaya n.k. …
… kwa habari zaidi tazama "dawa za asili"
Wamasai ni kabila lenye ufahari maalumu, na wasiokubali ushindi wa
kuendeleza mila yao utegemee hasa na misaada na neema kutoka kwa nchi tajiri
pekee, bali wajitegemee zaidi na uwezo wao wenyewe.
Kama ilivyo ni kawaidha kwa makabila wanaotimiza utamaduni wao wa asili, hata
wanawake wengi wa kimasai ni wataalamu wenye vipaji maalumu kwa kutengeneza kwa
mikono mapambo mbalimbali ya kimila. Kwa nia hiyo ya kiujitegemea wenyewe,
baadhi ya wanawake wa kimasai wanaoishi katika wilaya ya Simanjiro wanatengeneza
wenyewe baadhi ya mapambo maalumu, kama vile mikufu, shanga na bangili za ngozi
kwa kutumia vitu asili na shanga za rangi mbalimbali, ili wapate kuuzia kupitia
kukundi chetu cha „enkaina-e-retoto“…
… kwa habari zaidi tazama "duka letu"
„enkaina-e-retoto“ ni kikundi cha watu wasiokuwa na upendeleo na makanisa
wala madhebehu fulani na hakuna ushirikiano maalumu na watu wa dini yoyote. Bali
sisi tunapenda kuwaunga mkono tukiwa marafiki wa wamasai na utamaduni wao.
Vilevile tunayo nia ya kushirikiana kwa njia ya amani pamoja na makabila mengine
waishio Tanzania/Afrika ya Mashariki, ili nao wanufaike pia kutokana na miradhi
yetu kadhaa. Miradi yetu inayo malengo ya kupambana na njaa/umasikini, pengine
miradi yetu hulingana na matumaini makuu ya mamlaka ya mbuga za wanyama zilizo
karibu, yenye nia ya kuhifadhi mimea ya asili na wanyama pori - na kwa
hivyo miradi yetu ni muhimu mikoani na hata kwa mambo ya taifa...
… kwa habari zaidi tazama "washirikiaji wetu/Links"
Unayo maswali mengine ama mapendekezo fulani. Ama unapenda kubadilishana
mawazo kuhusu mambo yetu ya kuwaunga mkono wamasai, ama ukipenda kusaidia
kikundi chetu cha „enkaina-e-retoto“ kwa njia yoyote ile…?
… kwa habari zaidi tazama "mawasiliano"